Wakili maarufu aishitaki kampuni inayosambaza umeme,KPLC

Publish date: 2024-07-18

- Wakili maarufu ameishtaki kampuni inayosambaza umeme nchini,KPLC

- Apollo Mboya aliikashifu Kenya Power kwa kuongeza malipo ya umeme hasa mwezi wa Novemba na Disemba kwa kiwango kikubwa

- Wakenya wamekuwa wakilalama kuhusu ongezeko hilo ila hakuna hatua iliyokuwa imechukuliwa dhidi ya kampuni hiyo

Wakili maarufu,Apollo Mboya ameishtaki kampuni inayosambaza umeme,KPLC kwa niaba ya Wakenya wote kwa kuongeza malipo ya umeme.

Habari Nyingine: Picha za muuguzi huyu mwenye umbo la malaika zawapa 'mafisi' taabu

Kulingana na Apollo, kampuni hiyo iliongeza malipo hayo mwezi wa Novemba na Disemba ili iweze kufidia shilingi bilioni 8.1 ambazo ilikuwa imepoteza.

Apollo aliipa kampuni hiyo makataa ya siku saba kupunguza malipo hayo la sivyo hatua kali ya kisheria ichukuliwe dhidi kampuni hiyo.

Kama ilivyoripotiwa awali,Apollo alikuwa amewahimiza Wakenya kumtumia ushahidi wa kuonyesha ongezeka la malipo ya umeme ili aweze kuutumia kushtaki kampuni hiyo.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Wakenya wengi walituma malalamishi yao kupitia mitandao ya kijamii.

" Wakenya wenzangu,ili kupata ushahidi tosha wa kuishtaki kampuni ya umeme,KPLC,tafadhali tuma malalamishi yako kwa switchoffkplc@gmail.com’’, Apollo aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Habari Nyingine: Je, Akothee alimwoa meneja wake kwa harusi ya siri?

Aidha,Apollo aliwakikishia wakenya kwamba malalamishi yao yatatuliwa na kuahidi kuwajuza kila kunapozuka jambo lolote kuhusiana na kesi hiyo.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Pata habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia393fJZmrpqjmaG2brnAmqmunqVirqq%2Fx6KrmqOZYriiuc%2BupaJlmaOuurvSmqSbmaqWera5xKacpKicmHupwMyl